Kamwene! Kaka Maggid hizo picha ni hali ilivyokuwa kwenye kivuko cha Kilombero Jana jioni. Hali ni mbaya kwani kuna wananchi wengine wanavuka kwa kutumia mitumbwi na mto umejaa sana pia maji yana kasi kubwa. Sijui kwa siku ya leo hali ikoje huko mie niko zangu Mahenge nilivuka jana jioni kwa kiboti cha SUA ambacho kina injini nauli yake ni mia tano tu kama Loliondo. Hebu wahabarishe na wengine HII NDIO TANZANIAAnangisye Mwateba Mdau Mjengwablog |