Saturday, April 30, 2011

Vipaji Vingi Vyajitokeza Serengeti Filamu Jijini Arusha

Muigiza ji Hemed akiigiza na  mmoja wa waigizaji chipukizi waliojitokeza wakati wa kutafuta vipaji, katika Mwendelezo wa Dahabu na  Serengeti Fiesta Filamu  uliyofanyika leo kwenye klabu ya Mawingu jijini Arusha, mchakato huo ulianzia mkoani Mwanza, ambapo ulifanyika  kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupatikana kwa wasanii chipukizi lukuki ambao wanatakiwa kuendelezwa katika tasnia ya filam nchini.

Dada huyu anaonekana ni mtu mzima lakini naye ameamua kujitokeza na kuonyesha uwezo wake, katika kutafuta nafasi wakati wa  mchakato kutafuta vipaji vya uigizaji wa Serengeti Fiesta Filamu, uliofanyika leo kwenye klabu ya Mawingu jijini Arusha na kukutanisha vijana wengi wa jiji hilo.

Hapa wigizaji Hemed ambaye pia ni mwanamuziki akiigiza kwa umakini na Merry mmoja wa waigizaji chipukizi waliojitokeza katika mchakato wa Serengeti Fiesta Filamu, msanii huyo chipukizi ameeleza wazi kwamba anamkubali sana mwigizaji Aunt Ezekiel, kutokana na uwezo wake awapo kazini kwani amekuwa ni mvaa uhalisia halisi wa eneo ambalo analiwakilisha katika uigizaji wake.  (Fullshangweblog)