Saturday, April 30, 2011

JK Awaapisha Manaibu Makatibu Wakuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha John Thomas Mngodo, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi  wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi, baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana. Picha na Muhidin Sufiani- Ofisi ya Makamu wa Rais

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akifurahia na mtoto,  Irene Simba ambaye ni mtoto wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Juma Malemi (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete (katikati) Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakipiga picha ya kumbukumbi na Manaibu Makatibu Wakuu, baada ya kuapishwa rasmi kushika nyadhfa hiyo. Hafla hiyo ya kuapishwa ilifanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais