Sunday, April 24, 2011

Serengeti Fiesta Soka Soccer Bonanza Lafunika Mwanza; Mashabiki Wa Real Madrid Waibuka Washindi

Timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Hispania wa jijini Mwanza  imeibuka na ushindi wa jumla katika Tamasha la Mwendelezo wa Msimu wa  Dhahabu na Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililokutanisha mashabiki wa  vilabu mbalimbali vya Barani ulaya, ambalo limefanyika kwenye uwanja wa  CCM Kirumba Mwanza baada ya kuwafunga mashabiki wa timu ya Chealsea ya  Uingereza.
Mashabiki wa timu ya Real Madrid wa jijini Dar es  salaam pia walishinda na kuchukua kombe katika bonanza kama hilo  lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam hivi  karibuni.

Timu ya Mashabiki wa Chealsea iliyocheza fainali jana katika Bonanza la Serengeti Soccer jijin Mwanza


Hapa kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kikiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.

Mratibu wa Bonanza hilo Shafii Dauda wa pili kutoka kushoto akiongea na mashabiki kabla ya kukabidhi vikombe kwa washindi wa bonanza hilo, kushoto ni Khalfan Ngasa na kutoka kulia ni Meneja wa uwanja wa Kirumba Bw. Tegete na wa pili ni Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo.

Mashabiki mbalimbali wakisakata kiduku katika bonaza hilo. (Picha Zote kwa hisani ya Fullshangweblog)