Tuesday, April 26, 2011

Ripoti Ya Loliondo: Mdau- " Nikiwa Msomi, Nimeona Aibu Sana Kuisoma!"


Nimeona aibu sana nikiwa msomi baada ya kuisoma hiyo ripoti iliyoandikwa na hao wanaojiita wana PhD kuhusu dawa ya babu Loliondo. Yaani ni wazi kuwa hawakusoma hata hiyo ripoti yenyewe kabla ya kuichapisha na zaidi wametoa hoja za kipuuzi mno ukizingatia walivyo conclude hizo hoja.

Kwa ufupi hawakufanya chochote juu ya kuchunguza dawa ya babu kama inafanya kazi au hapana bali wameenda kutafuta taarifa kutoka katika vitabu vya watu na mitandao na kukopi bila hata kuchambua na kutoa conclusion za kitoto mno.

Yaani binafsi nasema hiyo ripoti waliyoitoa hata mtoto wa shule ya msingi hawezi conclude kama walivyofanya wao.

Nitatoa mifano miwili mitatu.
Unaposema kuwa dawa inavimelea vya kudhibiti (si kutibu) herpes simplex virus kwa hiyo inatibu HIV/AIDS yaani unanifanya nifumbe macho kwa aibu kwa kuwa ni wazi kuwa hufahamu HIV/AIDS ni nini na hujui tofauti kati ya hizo virusi mbili, na zaidi kwa kusema kuwa dawa hii inatibu Virus wa aina yeyote yule unamaanisha huji kabisa virusi ni nini kiasi hujui kuwa hakuna dawa ya kutibu hata virusi wa mafua, kwa ufupi hujui kuwa virus hawatibiki wakiingia mwilini, hakuna dawa ya kutibu virus yeyote yule aliye mwilini mwako hapa duniani.

Pili, watu wamekuwa wakiitumia hii dawa kote ulimwenguni na zaidi hapo hapo Tanzania, watu kama wamasai na wengine kama walivyotajwa kwenye ripoti wamekuwa wakiitumia hiyo dawa na hawajapona ukimwi wala hayo magonjwa mengine, iweje unasema kuwa dawa hii inatibu vitu hivyo?

Tatu, hawa wanaojiita ma PhD na ripoti yao wanaanzaje kusema kuwa mtu anapona kisukari au BP au Cancer? Ni wazi kuwa hata hawajui haya magonjwa ni nini? Eti kwa kuwa dawa ina elements kama Metformin na kadharika inatibu kisukari, jamani hizi element mnazozitaja hamna hata moja inatibu kitu hapo bali zinapunguza tu makali ya ugonjwa kwa muda unaotumia hizo elements na ukiacha tu ugonjwa upo palepale, iweje unasema dose ya babu inatibu eti kwa kuwa ina hizo elements wakati kwanza mtu anakunywa mara moja tu?

Binafsi sijawahi kuona kikombe chenye 200 mils kikombe kimoja ni sawa na 30 mils (1 cup = 30 mils), hizo hesabu zao wamezitoa wapi.

Haya ni baadhi tu ya ujinga ulioandikwa humo, sina muda wa kuchambua ripoti nzima hapa maana tunaweza tukaandika kitabu.

Yaani hawa ndiyo wataalamu wetu Tanzania? Kweli ndiyo watu mnashabikia kuwa eti watanzania wasomi? PhD hizi, PhD gani jamani. Hili ni janga kwa taifa nawaambia.