Saturday, April 30, 2011

Olimpiki Maalumu Wanaomba Msaada Wa Tiketi 5 Za Wachezaji Kwenda Ugiriki

       Mkurugenzi wa Olimpik Maalumu Frank Macha.                                                                                                                                      Wachezaji wenye ulemavu wa akili  11 wamechaguliwa kushiriki mashindano ya riadhaa ya DUNIA nchini UGIRIKI ambayo yamepangwa kufanyika JUNE mwaka huu.        
Mkurugenzi wa Olimpiki Maalumu ameseama kuwa  mpaka sasa wamepata tiketi sita tu  kati ya tiketi kumi na moja zinazohitajika kufanikisha safari ya wachezaji hao. Bado tiketi tano kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo ,hivyo Mkurugenzi huyo anawaomba watu wenye uwezo wa kuwasaidia wachezaji hao wajitokeze kutoa msaada wa vifaa vya michezo nguo kwa ajili ya safari pamoja na tiketi ili kufanikisha safari ya wachezaji hao wenye ulemavu wa akili.

Amesema iwapo watashindwa kupatiwa msaada huo watapeleka wachezaji wachache tu ,wachezaji hao mpaka sasa wanaendelea na mazoezi  nje ya kambi kabla ya kuondoka nchini kwenda Ugiliki kwenye mashindano hayo ya Dunia June mwaka huu.