Ndugu,
Salaam katika upendo
Hii ni kuwajulisha kuwa mtandao mkubwa wa habari ujulikanao kama http://thehabari.com umeanzishwa kwa kushirikiana na baadhi ya wanataaluma wa tasnia ya habari nchini Tanzania na baadhi ya wanahabari kutoka Tanzania walioko Los Angeles, Marekani kwa shughuli mbalimbali. Mtandao huu ulianza kazi tangu Novemba mwaka 2010 na sasa unaendelea kuongeza wadau na wachangiaji ili kukidhi malengo ya mtandao.
The Habari.com ni mtandao wa kizalendo unaokuletea habari za kijamii, kisiasa, burudani na teknolojia. Tupo hapa kushirikiana na waTanzania wenzetu popote walipo duniani katika kuelimishana na kufahamishana mustakabali mzima wa nchi yetu. Tumedhamiria kuleta habari kwa uwazi na umakini bila uwoga wala upendeleo wa aina yeyote.
Tuna amini katika falsafa ya habari kuwa habari ni watu na watu wenyewe ndiyo sisi, hivyo basi tushirikiane katika kuendeleza gurudumu la maendeleo katika nchi yetu tuipendayo ya Tanzania.
Ukiwa kama mdau unakaribishwa kutuma, kutoa taarifa, kuchangia ushiriki na hata kutoa maoni yako. Asante kwa kupokea. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi;
Joachim Mushi
Mhariri wa The Habari.com Tanzania
0717030066, 0756944670,
Mail; mushi@thehabari.com
Or tembelea; joemushi.blogspot.com
|
|
|---|