Wednesday, April 27, 2011

Diwani Aliyemita Chiligati Fisadi Sasa Amgeukia Mbunge Wa Jimbo La Kalenga

SAKATA la diwani wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Mgama wilaya ya Iringa vijijini Denis Lupala (pichani) ambaye alimwita naibu katibu mkuu wa CCM bara kepteni John Chiligati kuwa ni fisadi limeendelea kuchukua sura mpya ndani ya CCM baada ya diwani huyo sasa kumvaa mbunge wa jimbo la Kalenga Dr.Wiliam Mgimwa kuwa amekuwa akiendekeza makundi na kutaka chama kumvua magamba.
Akizungumza namtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com Lupala alisema kuwa upo uwezekano wa serikali ya CCM iliyopo madarakani kuendelea kuchafuliwa na viongozi wake na kutoa nafasi kwa vyama vya upinzani kama chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) kuendelea kupata umaarufu kutokana na wale waliochaguliwa kuendeleza chuki za kura za maoni ndani ya CCM.
“Ujue wapo wabunge ambao hawaamini kama wamekuwa wabunge na hawaamini kama uchaguzi mkuu umemalizika ...wabunge hawa ndio ambao bado wanaendekeza makundi hadi sasa kwa kuwachukia wale waliokuwa upande wa wagombea wengine wakati wa mchakato…mfano mbunge wetu wa jimbo la kalenga Dr.Mgimwa yeye bado anaendelea kuwatumia wapambe wake kwa kila jambo na kuwatenga wale ambao hawakuwa upande wake" (Imeandikwa na Francis Godwin)