Sunday, May 1, 2011

Kuna Kuchambua, Kupembua Na Kupelemba!




Napenda kuchambua mboga za majani. Ninapochambua huchambua pia fikra zangu. Na kuna tofauti ya kuchambua, kupembua na kupelemba. Unazijua?
Pichani nachambua majani ya maboga. Kisha nikaandaa mboga ya maboga kwa mlo wa mchana wa leo . Mboga iliyochanganywa na uyoga, bamia, nyanya chungu na pilipili shamba. Na utamu wake? We acha tu!