Abiria walionusurika katika ajali hiyo MAMA na mtoto wamefariki dunia papo hapo huku abiria 30 wakijeruhiwa baada ya basi waliokuwa wakisafiria la kampuni ya Al-Saedy lililokuwa likitoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam kupata ajali iliyohushwa na lori na kupinduka eneo la Sangasanga kwa Mwarabu katika wilaya ya Mvomero barabara kuu ya Iringa-Morogoro mkoani hapa. Ajali hiyo ilitokea Majira ya 11:45 jana jioni katika eneo hilo Ambapo basi lenye namba ya usajili T 267 AWG Scania mali ya kampuni ya Al-Saedy yenye makao makuu mkoani Morogoro ilikuwa linaendeshwa na dereva Erick Luoga ikitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam iligongana na lori lenye namba ya usajili T 346 ABX Scania likiwa na tela T 657 AGU mali ya kampuni ya Trans Cargo ya Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na dreva, Ally Khamis (48) mkazi wa Kigogo Jijini Dar es Salaam ilisababisha vifo vya abiria wawili ambao ni mama na mtoto wake.(Habari na Picha: Juma Mtanda) |